Michezo Mingine

Mataifa saba kuchuana PickelBall

DAR ES SALAAM : ZAIDI ya Mataifa Saba Duniani ikiwemo Kenya,Congo ,Rwanda ,Uganda,South Afrika ,Dubai kuja Nchini kwa ajili ya mashindano ya mchezo wa PickeBall yatakayoanza tarehe 27 hadi 31 mwezi huu.

Hayo ameyasema leo Rais wa Chama Cha Pickeball Kartik Kapoor Nchini Tanzania na kusema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika viwanja wa Gymkhana jijini dar es salaam na kusema kuwa michezo ni fursa hivyo watu wajitokeze kushiriki Kwani wanabadilishana uzoefu.

Aidha Kapoor amesema kuwa mashindano hayo ni makubwa na Tanzania imepata wasaha kufanyika hivyo yana tija na manufaa kwa Taifa na Jamii kwa ujumla.

Kwa Upande wao makocha wa mchezo huo Mathew David na Peter Kally wamesema mchezo huo sio lazma uwe na viwanja maalum na imara Kila sehemu Bali unaweza kufanyika popote na kwa sasa Kuna baadhi ya mikoa kama kagera na morogoro wanacheza .

Nao wachezaji wa mchezo huo Sall Odak na Edna Mfinanga wamesema wamejipanga vyema na mchezo huo hivyo wanatajia kushinda na kupata fursa zaidi.

Related Articles

Back to top button