Michezo Mingine

Mpango kufanya mazoezi nchi nzima waja

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwa na mpango wa kufanya mazoezi ya viungo nchi nzima, utakapokamilika utatangazwa.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa alisema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika Viwanja vya Gymkana Dar es Salaam.

Msigwa alisema katika mpango huo, wizara yake itashirikiana na Wizara ya Afya kuratibu ili kila mtanzania aweze kushiriki.

“Naombeni tufanye mazoezi, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, tunakuwa na mpango mkubwa wa mazoezi nchi nzima,

” Tukija na hiyo program naomba watanzania tuunge mkono tujenge tabia ya kufanya mazoezi,” alisema.

Msigwa alisema kwa kufanya mazoezi kutawezesha kuwa na afya bora pamoja na kupunguza maradhi.

“Tuepuke vidonge, waganga tufanye mazoezi ili tuwe na afya nje. Ukiwa na afya nzuri utajenga uchumi wa taifa na familia,” alisema.

Alisema Yoga ni sehemu ya mazoezi ambayo ni muhimu ya kuujenga mwili vizuri, hivyo alishauri watanzania kujifunza Yoga iwasaidie kwa afya.

Awali Mwakilishi wa Balozi wa India nchini, Manor Verma alisema maadhimisho haya ni awamu ya 10, ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 21 kila mwaka ulimwenguni.

Alisema watanzania wengi wameungana na India kueneza ujumbe wa Yoga.

Alitaja kauli mbiu ya mwaka huu kuwani, Yoga kwa ajili ya mtu binafsi na jamii nzima,”.

Alisema mazoezi ya Yoga yanahusisha namna ya kupumua, mazoezi ya shingo, mikono na viungo pamoja na tafakari

Related Articles

Back to top button