Michezo Mingine

Bonanza la TASWA Desemba 9

TAMASHA maalum kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoka vyombo vya habari ‘TASWA Media Day Bonanza’ linatarajiwa kufanyika Dar es Salaam Desemba 9, 2023.

Taarifa ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo(TASWA) imesema lengo la bonanza hilo linaloandaliwa na chama hicho ni kuwaweka pamoja waandishi wote ili kubadilishana mawazo na kufurahi.

TASWA imesema tamasha hilo litawakutanisha waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya au mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Taarifa hiyo imesema tayari wadau mbalimbali wameafiki kudhamini bonanza hilo ambapo mazungumzo yapo hatua za mwisho.

Related Articles

Back to top button