Ligi Kuu

Maskini Yanga limewakuta jambo

Dube majeraha yambakiza Dar

DAR ES SALAAM: Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Prince Dube, amelazimika kubaki Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi kufuatia kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya TRA uliochezwa jana.

Kamwe amesema wakati Dube akibaki jijini Dar es Salaam kwa uangalizi wa kitabibu, kikosi cha Yanga tayari kimewasili Dodoma kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa Machi 21 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kuumia kwa Dube ni pigo jipya kwa Yanga ambayo tayari inakabiliwa na wimbi la majeruhi ndani ya kikosi chake.

Baadhi ya wachezaji waliokosekana tangu mchezo uliopita ni pamoja na Laurindo Aurelio ‘Depu’, Chadrack Boka, Ibrahim Bacca na Edmund, wote wakiwa nje kutokana na majeraha.

Aidha, wapo pia wachezaji wanaokabiliwa na majeraha ya muda mrefu akiwemo Dickson Job pamoja na Clement Mzize, hali inayozidi kuipa changamoto benchi la ufundi la klabu hiyo kuelekea michezo ijayo.

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa imetoka kupata sare mbili mfululizo dhidi ya TRA na Azam FC, matokeo yanayoongeza presha kwa timu hiyo kutafuta ushindi ili kuendelea kujiweka kileleni nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.

Related Articles

Back to top button