Nyumbani

Amoah na Azam FC ni hivi

DAR ES SALAAM: Uongozi wa Klabu ya Azam FC umetangaza kutemana na aliyekuwa beki wao Daniel Amoah raia wa Ghana.

Amoah alikuwa moja ya wachezaji waliohudumu kikosini hapo kwa muda mrefu kwani alijiunga na matajiri hao wa Kusini mwa Dar es Salaam mwaka 2016.

Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za klabu hiyo leo imesomeka kama ifuatavyo
#ThankYou Ahsante kwa utumishi wako wa miaka nane ya nguvu ukiipigania nembo ya klabu yetu, aliyekuwa nahodha wetu, Daniel Amoah.

Thank you for your memories, Amoah! 👍🤝👏imemalizika taarifa hiyo.

Amoah amefuata nyayo za nyota Prince Dube aliyetangaza kuachana na timu hiyo tangu msimu uliopita licha ya kwamba Azam FC wamesisitiza kuwa bado wana mkataba nae.

Related Articles

Back to top button