Afrika Mashariki

Marioo, Matata kutangaza utamaduni wa Afrika kupitia ‘Nyongi’

 

NAIROBI: MSANII wa Tanzania Omary Mwanga ‘Marioo’ ameungana na kundi maarufu la muziki wa pop kutoka Kenya, Matata na wameachia wimbo wao unaoitwa nyongi.

Wimbo huo ni utangulizi wa EP ya kundi hilo itakayoitwa ERA (East Rise Again) inayotarajiwa kutoka mwezi Juni ikiwa na nyimbo sita pamoja na wimbo wa ‘Kanairo’ unaotarajiwa kutoka Mei 2026.

Wimbo ‘Nyongi,’ umetayarishwa na mtayarishaji wa Kenya Wodomolo, unamchanganyiko wa ladha ya muziki wa pop ya Kenya na miondoko laini ya Bongo Fleva kutoka Tanzania ambazo zimeunda sauti ya kuvutia yenye midundo ya kisasa ya Afrika Mashariki.

Wanamuziki wa Kundi la Matata walisema:
“Kulikuwa na kitu cha kipekee tulipofanya kazi na Marioo. Tuliingia studio Nairobi na kutoka na wimbo unaozidi ukubwa wa namna tulivyotarajia. Ni Sheng imekutana na Bongo Fleva, Nairobi imekutana na Dar es Salaam nguvu na tukio maalum limetokea kati yetu hilo ni la kujivunia mno.”

Marioo naye alisema:
“Kufanya kazi na Matata ilikuwa uzoefu wa kipekee. Nguvu yao na mtindo wao wa kipekee umeleta kitu maalumu kwenye wimbo huu. ‘Nyongi’ inaleta maana halisi ya uhusiano mkubwa wa muziki wa Afrika Mashariki.”

Marioo amekuwa na utaratibu wa kushirikiana na wanamuziki kutoka keenya ambapo aliwahi kushirikiana na mwanamuziki kutoka Kundi la Sout Soul, Bien.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button