Muziki

Mapana alia na wasanii

DAR ES SALAAM: KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk. Kedmon Mapana amewataka Wasanii nchini kuwa kioo cha Jamii kwa kufanya kazi zao na kuangalia mila na desturi.

Akizungumza na wahandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Dk. Mapana amesema wasanii wanatakiwa kufanya kazi zao za sanaa kwa kufuata mila na desturi huku wakiwa mabalozi wazuri katika kueneza na kudumisha utamaduni wa nchi yetu ya Tanzania.

“Wanatakiwa kuangalia na kuzingatia Mila zetu zipoje wanapoandaa kazi zao na kujua Zina manufaa gani kwenye jamii mara baada ya kusikiliza nyimbo zao,itasaidia kulinda Mila na tamaduni zetu.

“Unapofanya kazi unatakiwa kuangalia ina manufaa gani kwenye jami. Unatakiwa kwa makini kabla ya kuiachia katika mitandao, unapaswa kufuata tamaduni zetu.” Amesema Dk. Mapana

Related Articles

Back to top button