EPLKwingineko

Man UTD yamhitaji Mount kwa bil 158/-

MASHETANI Wekundi wa Old Trafford, Manchester United imeanzisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Mason Mount kwa pauni milioni 55 sawa na shilingi bilioni 158.6.

Nyota huyo wa kimataifa wa England ni lengo kuu la usajili la kocha Erik ten Hag kuelekea dirisha la uhamisho la majira ya joto na bosi huyo wa United anataka dili hilo likamilike haraka.

Mount anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake Stamford Bridge huku utata wa hatma yake ukiongezeka.

Vyanza vya habari vya Old Trafford vimeonesha kuwa mazungumzo kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 yanatarajiwa kuanza.

United inataka kulipa pauni milioni 55 kiasi ambacho ni chini ya uthamini wa Chelsea wa pauni milioni 85 sawa na shilingi bilioni 245.

Related Articles

Back to top button