Tetesi

Simu ya Azam yaita ‘Straika’ Uganda

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Vipers. Allain Okelo lengo la kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimu ujao Azam FC, wataungana na Yanga kwenda kuwakilisha nchini katika michuano hiyo baada ya timu hiyo kumaliza Ligi Kuu Bara wakiwa katika nafasi mbili za juu.

Taarifa zilizoifikia Spotileo ni kuwa, viongozi wa Azam FC, wamekuwa wakiwasiliana na mawalaka wa Okelo kuangalia namna ya kupata huduma ya nyota huyo msimu ujao.

Chanzo hicho cha kuaminika kimesema kiungo mshambuliaji huyo yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na matajiri hao wa Chamazi, kuimarisha zaidi kwenye safu ya kiungo kutokana na mashindano yaliyopo mbele yao.

“Okelo ni mchezaji mzuri ameonesha kiwango bora kwenye ligi ya Uganda ni Fei Toto, mwingine, Azam FC wanaendelea kufanya mazungumzo na Vipers kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupata huduma ya nyota huyo,” anasema mtoa habari huyo.

Hata hivyo, Azam itakuwa na ushindani, kwani klabu zingine ikiwemo El Marrikh kutoka Sudan na Stellenbosch ya Afrika Kusini ambao wameonyesha nia ya kuhitajika huduma ya kiungo mshambuliaji huyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit aliahidi usajili mzuri kuboresha timu kwa kufuata mapendekezo ya kocha wao, Youssouph Dabo kuimarisha kila eneo ndani ya kikosi kwa msimu ujao wa mashindano yaliyopo mbele yao.

Related Articles

Back to top button