Tetesi

Chelsea yaiongoza Arsenal kumsajili Osimhen

Chelsea ipo mbele ya Arsenal katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Napoli raia wa Nigeria Victor Osimhen,25, majira yajayo ya kiangazi. (Teamtalk)

Real Madrid inapanga kuhuisha kipengele cha kuachiwa cha Erling Haaland mwaka ujao lakini Manchester City ina matumaini ya kumfunga kwa mkataba mpya ifikapo kipindi hicho ambao utaondoa kipengele hicho. (Fichajes – Spain)

Pia agenda ya Real Madrid katika klabu ya Paris Saint-Germain ni kumsajili beki wa kulia Achraf Hakimi, ambaye anataka kuondoka miamba hiyo ya Ufaransa. Man City pia ina nia kumsajili. (Sports Zone – France)

West Ham inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth raia wa England Dominic Solanke,26.

Bayern Munich itashindana na Liverpool katika kumteua kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso kuwa kocha wa timu hizo. (Guardian)

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane atarejea katika kazi ya ukocha kuchukua mikoba Bayern Munich. (Sport – in German)

Related Articles

Back to top button