Tetesi

“Hatuna ishu na Fei Toto” – Ahmed Ally

DAR ES SALAAM: MENEJA wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amekanusha tetesi za klabu hiyo kumtaka kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa msimu huu wa 2024/25 wa Ligi Kuu Bara na mashindano ya Kimataifa.

Simba ipo kwenye matengenezo ya timu imara kwa kufanya usajili wa kuwa na kikosi bora kwa ajili ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu msimu ujao, baada ya msimu ulimazilika kushika nafasi ya tatu na kwenda kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho.

Ahmed ameiambia Spotileo kuwa wanatambua uwezo na kiwango bora cha Fei Toto na hakuna timu inauwezo wa kumkataa lakini wao kama Simba hawana mpango na mchezaji huyo.

Amesema Simba imenyooka wakihitaji mchezaji hufuata taratibu zote ikiwemo kuzungumza na klabu husika juu inayomiliki kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mchezaji baadae kusajiliwa.

“Hizo ni tetesi, hakuna ukweli wowote juu ya Kamati ya Usajili au kiongozi wa Simba wakimtaja Fei Toto, kama tungemuhitaji mchezaji huyo tungefanya maamuzi ya kuzungumza na Azam FC, juu ya biashara,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa uongozi wa Mwenyekiti Mohammed Dewji (Mo) hakuna mchezaji anayetakiwa na Simba akashindwa kusajiliwa, wangemuhitaji Fei Toto wangefanya mchakato wa kumsajili.

Ahmed amesema wachezaji walitakiwa wote wamesajiliwa na wanaingia kambini na Jumatatu watakuwa safarini kuelekea nchini Misri kwa ajili ya maandalizi wa msimu mpya wa mashindano.

Related Articles

Back to top button