Mama wa Kim Kardashian aondolewa kizazi

MAMA wa mwanamitindo Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 68 aliangua kilio wakati alipokuwa akiiambia familia yake kwamba alihitajika kuondolewa kizazi chake baada ya madaktari kugundua uvimbe mdogo sehemu ya kizazi chake.
Akizungumza katika kipindi cha hivi karibuni cha ‘The Kardashians’, Kris aliwaambia marafiki zake Kathy Hilton na Faye Resnick: “Nitafanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi.
“Madkatari wamenishauri niondolewe uvimbe kwa upasuaji ili uvimbe huo usikue na kuleta madhara zaidi,” alisema
Lakini katika tangazo la kipindi kijacho cha Julai 18 cha ‘The Kardashians’, Kris anaonekana akiwashukuru madktari na kuwapa taarifa mashabiki wake kwa kufanikisha upasuaji wake na kwamba anajisikia vizuri.
Kris mwenye watoto sita, Kourtney Kardashian (45), Kim Kardashian (43), Khloé Kardashian (40), Rob Kardashian (37), Kendall Jenner (28) na Kylie Jenner (26) amekiri kuwa kabla ya upoasuaji huo alikuwa na hofu inawa alimwamini mno daktari wake aliyemfanyia upasuaji huo.
Awali Kris alionekana akiangua kilio kwenye kipindi cha televisheni alipowakusanya Kim, Khloe na Kendall na kuwafahamisha watoto wake hao kwa hisia kuhusu uvimbe uliopatikana sehemu yake ya kizazi.
Aliwaambia: “Nilitaka kuwaambia nyinyi kitu kwa sababu nilikuwa bado sijawaambia, mnajua nilienda kwa daktari na nikafanyiwa uchunguzi wangu, waligundua uvimbe mdogo kwenye ovari yangu,” watoto wake walihuzunishwa na taarifa hiyo ya awali.