Masumbwi

Mabondia wanawake kuchuana Tanga

 

DAR ES SALAAM: Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limetangaza kuandaa mashindano maalum ya ngumi kwa wanawake yatakayofanyika Aprili 6 na 7 mwaka huu mkoani Tanga.

Akizungumza na SpotiLeo, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, amesema mashindano hayo awali yalipangwa kufanyika mwezi huu lakini yalilazimika kusogezwa mbele kutokana na kipindi cha Ramadan.

Mashaga amesema baada ya mashindano hayo ya wanawake kumalizika, shirikisho hilo pia litaandaa michuano mingine ya kuwania ubingwa wa Taifa kwa wanaume na wanawake itakayoanza Aprili 16 mwaka huu.

Amesema lengo la mashindano hayo ni kupata mabondia watakaounda kikosi kipya cha Timu ya Taifa ya Ngumi Tanzania kitakachoiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

“Tumeandaa mashindano haya kwa lengo la kuibua vipaji vipya na kuchagua mabondia watakaoingia kwenye timu ya Taifa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa,” amesema Mashaga.

Aidha, amesema tayari wamepeleka mialiko katika mikoa mbalimbali nchini ili kuwahamasisha mabondia kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano hayo muhimu.

 

Related Articles

Back to top button