Masumbwi

Msigwa: Mchezo wa ngumi upo mikono salama

DAR ES SALAAM: KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema Serikali inaendelea kuunga mkono wadau wa michezo hasa wa ngumi ili kuendelea kufanya vizuri na kuwa mchezo pendwa hapa nchini.
Msigwa ataungana na bosi wake Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo, Damas Ndumbaro kushuhudia pambano la ngumi la Dar Boxing Derby Jumamosi ya Juni 29, mwaka huu, katika viwanja vya Kijitonyama, jijijini.
Msigwa ameiambia SpotiLeo kuwa, Serikali inaendelea kuunga mkono wadau wote wa ngumi katika kuendeleza mchezo huo na jitihada hizo hazitakiwi kupuuzwa kwa kuwa miaka ya nyuma mchezo huo ulifanya vizuri zaidi.
“Sasa Mabondia wetu wanacheza mapambano mengi ya ndani tafsiri yake kazi kubwa imefanyika kuhakikisha mazingira ya mchezo yanafanyika, mabondia wamekuwa wakifanya kazi kubwa hata wakienda nje kushiriki mashindano licha ya uwepo wa baadhi ya mapungufu katika maandalizi yao,” amesema Msigwa.

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza mdau wa Masumbwi Selemani Semunyu kwa kazi kubwa anayoifanya na Serikali haitamuacha peke yake, ili kukabiliana na changamoto ya maandalizi mipango ya baadae ni ujenzi wa Gym ya Kisasa na kutumiwa na mabondia wote.

“Niwaombe wananchi wote wapenda michezo wajitokeze siku hiyo ya Juni 29, mwaka huu kujionea burudani adhimu,” amesema Katibu huyo wa Wizara.

Naye Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto alisema licha ya kushiriki kama mtazamaji pia atashiriki katika maandalizi ya pambano hilo.

Pambano kuu siku hiyo ni Kati ya Nassibu Ramadhani dhidi ya Juma Choki.

Related Articles

Back to top button