Lupita Nyong’o apewa dili la filamu ya kuchekesha
LOS ANGELES: MUIGIZAJI Lupita Nyong’o aliyetamba katika filamu ya ’12 Years a Slave’ amelamba dili nono linguine la kuigiza filamu lakini kwa sasa ataigiza katika filamu ya vichekesho.
Lupita mwenye miaka 41 anasema tangu alipocheza filamu ya ‘12 Years a Slave’ amekuwa akipokea madili mengi ya kucheza katika filamu mbalimbali na amekuwa akitamani kucheza filamu za vichekesho.
Lupita, ambaye alishinda tuzo ya muigizaji msaidizi bora katika tuzo za Oscar kwa kazi yake mwaka wa 2013 aliwambia mashabiki wake kwamba amekuwa nah amu ya kushiriki katika filamu tofauti tofauti ili aonyeshe uwezo wake sehemu tofauti.
“Sipati nafasi za kuchea katika filamu za vichekesho. Najulikana kwa kucheza filamu nyingi. Siku zote ninajaribu kuchagua majukumu ambayo sijacheza hapo awali, majukumu ambayo yataonyesha uwezo wangu wa nafasi nyingine katika uigizaji” alifafanua.
“Nadhani vichekesho vinatisha sana. Ni vigumu sana kufikia na ninataka kujaribu zaidi kucheza filamu hizo.” Alisema.