Tetesi

Baleke awaita mezani wanaomhitaji

DAR ES SALAAM: ALIYEKUWA Mshambuliaji wa Simba na sasa anakipiga katika klabu ya Al Ittihad ya Libya,Jean Baleke ameziita mezani timu zinazohitaji huduma yake kuwa yupo tayari kurejea kucheza Tanzania endapo atapata ofa nzuri.

Baleke yupo nchini na jana alikuwepo uwanja wa Azam Complex, Chamanzi akishuhudia mechi ya Simba Queens na Fountain Gate Princess na anahusishwa kuzungumza na timu mbili zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, Yanga na Azam FC kuwa wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Akizungumza na Spotileo, Baleke amesema hakuna mazungumzo na kiongozi yoyote kati ya Yanga au Azam FC ambao anafanya nao mazungumzo na yupo nchini kwa ajili ya mapumziko baada ya kutamatika kwa ligi ya Libya.

Amesema hakuna jambo la kushangaza kwakuwa aliwahi kucheza Tanzania, kunako klabu ya Simba yupo nchini kwa ajili ya mapumziko na kwenda kushuhudia Simba Queens ikicheza mechi pamoja na baadhi ya mabosi wake wa zamani.

“Niko Tanzania katika mapumziko, nilienda Azam Complex kuangalia Simba Queens, hapa ni sehemu ya nyumbani, sijapigiwa simu wala kutafutwa na kiongozi yoyote anayenitafuta na kuhitaji huduma yangu kwa msimu ujao,” amesema Baleke.

Mshambuliaji huyo aliitumikia Simba misimu miwili kwa mkopo akitokea TP Mazembe ya DR Congo na aliondoka kipindi cha dirisha dogo akiwa na mabao nane na kutimkia katika klabu ya Al Ittihad ambako nako yupo kwa mkopo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button