Tetesi

Mbappé bado aitikisa PSG

TETESI za usajili zinasema fowadi wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappé, 25, na kambi yake hawajashawishika na ofa ya hivi karibuni ya Real Madrid ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye atakuwa huru kusajiliwa klabu nyingine majira yajayo ya kiangazi kwani ni chini ya ofa iliyotolewa Mei 2022. (Athletic – subscription required)

Kiungo wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29, ni mlengwa wa usajili katika timu ya Paris Saint-Germain, huku mabingwa hao wa Ufaransa wakikusudia kulipa pauni mil 51 za kuachiwa mchezaji huyo. (Fichajes – in Spanish)

Arsenal na Liverpool zote zina nia kumsajili winga wa Ureno Pedro Neto,23, toka Wolves, ambayo inakusudia kumuuza iwapo zitatimiza masharti ya thamani yake kwa sababu ya shinikizo la kifedha.(Fichajes – in Spanish)

Wolves itataka karibu pauni mil 50 hadi 60 kwa ajili ya Neto, ambaye ana mkataba Wolves hadi 2027. (Football Insider)

Chelsea inamfuatilia beki wa kushoto wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 20, pamoja na beki wa kati wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23. (Football Transfers)

Kocha wa Bayern Leverkusen Xabi Alonso sasa anawindwa na Barcelona pamoja na Real Madrid na Liverpool. (Sport – in Spanish)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button