Tetesi

Man UTD, PSG zaongoza mbio kumsajili Osimhen

TETESI za usajili zinasema Manchester United na Paris Saint-Germain zinaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen, 25, majira yajayo ya kiangazi.

Arsenal na Chelsea pia zimeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Nigeria. (Independent)

Liverpool huenda ikailipa Bayer Leverkusen ada ya kuvunja rekodi ya pauni mil 21 kumteua Xabi Alonso kuwa kocha Anfield majira yajayo ya kiangazi-mara mbili zaidi ya iliyolipa kumsajili mhispania huyo akiwa mchezaji. (Mirror)

Wachezaji kadhaa wa Manchester United wanaamini nafasi ya kocha mdachi Erik ten Hag itajazwa mwisho wa msimu.(Mail)

Tottenham Hotspur imepeleka maskauti kumfuatilia kiungo wa Denmark anayekiwasha Sporting Lisbon, Morten Hjulmand, 24.(Record, via Sun)

Related Articles

Back to top button