Ligi KuuNyumbani

Ligi Kuu yashika kasi

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kushika kasi huku michezo minne ikipigwa leo Mwanza, Geita, Mbeya na Singida.

Kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Singida Fountain Gate inayoshika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 baada ya michezo 17 itakuwa wenyeji wa Azam iliyopo nafasi ya 2 ikiwa na pointi 37.

Kagera Sugar inayoshika ya nafasi ya 8 ikiwa na pointi 21 itakuwa mgeni wa Geita Gold iliyopo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 16.

Kwenye uwanja wa CCM Liti mjini Singida, Ihefu inayoshika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 19 ambayo ilimehamia mkoani humo itaikaribisha Mashujaa iliyopo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 14.

Tabora United iliyopo nafasi 13 ikiwa na pointi 18 itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons iliyopo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 21 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Related Articles

Back to top button