Nyumbani

Kuiona Stars kwa mkapa buku 2 tu!

DAR ES SALAAM: OFISA habari wa shirikisho la soka nchini TFF Clifford Ndimbo Ametaja viingilio vya mchezo wa marudiano wa kufuzu kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2025, huku eneo la mzunguko likiwa ni shilingi elfu mbili tu za kitanzania

Ndimbo amesema sababu ya kuweka kiingilio hicho ni kuvutia mashabiki wengi zaidi kuipa hamasa timu ya taifa ili iweze kushinda mchezo huo dhidi ya DR Congo utakaochezwa Jumanne Oktoba 15 saa moja usiku uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kujiweka kwenye nafasi ya kufuzu.

“tumezingatia eneo hilo kwa sababu ndio eneo linabeba mashabiki wengi zaidi, hata kwenye maeneo yanayobeba mashabiki wachache kiingilio cha juu ni elfu 5 na hayo ni maeneo ya VIP B na C kwa hiyo utaona ni kwa namna gani ni viingilio rafiki”.

“Kwa hiyo utaona ni kwa namna gani ni viingilio rafiki, njooni tuwasapoti nyota wetu ambao wanapambana kwa ajili ya bendera ya taifa letu” amesema Ndimbo

Taifa stars ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Congo kwa bao moja bila majibu jijini Kinshasa nchini Congo Oktoba 10 mwaka huu na watarudiana Oktoba 15 Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button