Nyumbani

Samia mgeni rasmi Simba Day

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha wiki ya Simba, Simba Day Agosti 6.

Wakati wa kilele hicho Simba inatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos kutoka Zambia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Karibu kwenye kilele cha Wiki ya Simba. Karibu kwenye Simba Day, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii ni siku muhimu kwa Klabu ya Simba na wapenda michezo wote nchini Tanzania,” imesema taarifa ya Simba.

Simba imemshukuru Rais Samia kwa mchango wake mkubwa kwenye sekta ya michezo na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button