Masumbwi

‘Knockout ya Mama season 2’ yawapeleka mabondia ‘Sauzi’

DAR ES SALAAM: MABONDIA wa Kampuni ya promosheni ya ngumi za kulipwa nchini, Mafia Boxing Promotion, Ibrahim Mafia ‘Mafia Tank’, Saidi Chino, Salmini Mizinga na Kalolo Amiri wamesafiri chini mchana wa leo kwenda Afrika Kusini.

Mabondia hao wanaenda kwa lengo la kuweka kambi ya maandalizi ya pambano Knockout ya Mama kwa msimu wa pili inayotarajia kufanyika Desemba 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuondoka mabondia hao wamesema kuwa watatumia vizuri kambi hiyo kwa lengo la kuendelea kupeperusha bendera ya nchini kimataifa kwa kushinda mapambano ya mkanda wa ubingwa.

Licha ya mabondia hao kutaka kupeperusha bendera lakini pia kupata fedha za motisha ya Knockout ya mama zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Related Articles

Back to top button