Masumbwi

Rais Samia atoa Mil 5 kwa Ubaya

DAR ES SALAAM: RAIS Dk Samia Suluhu Hassan amemzawadia Sh milioni 5, bondia mtanzania Abdul Ubaya.
Kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amemkabidhi kiasi hicho cha fedha bondia huyo kwa kushinda wa Knockout ya raundi ya pili nchini Urusi.

Ubaya ameshinda pambano hilo la raundi sita katika uzani wa Light Heavy kwa kumchapa Ibragim Estemirov lililofanyika Oktoba 25, 2024 nchini Urusi.

Msigwa amesema Rais Samia ametoa fedha hizo kwa lengo la kuongeza hamasa kwa vijana kujituma katika kuipeperusha bendera ya Taifa vizuri.

Bodia huyo amemshukuru Rais kwa kutambua mchango wa mabondia na kuweka kiasi cha fedha kwenye ngumi (Knockout Ya Mama) ambayo inatoa hamasa kwa vijana kwenda kupambana.

“Tunaenda kuwakilisha Taifa lakini hii Knockout Ya Mama inaleta hamasa kwa vijana kwenda kucheza mapambano ya kimataifa nje na kutafuta ushindi lakini kupata fedha za Rais Samia “ amesema Ubaya.

Related Articles

Back to top button