Changalawe ampiga Mnigeria
ABUJA: Bondia wa timu ya Taifa Yusuf Changalawe ameshinda pambano lake la hatua ya robo fainali dhidi ya Solomon Jegede kutoka Nigeria katika michezo ya pili ya Majeshi ya Afrika inayofanyika katika mji mkuu wa Abuja, Nigeria.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Lukelo Willilo Changalawe alishinda raundi ya tatu baada ya mwamuzi kusimamisha pambano kufuatia mpinzani wake kuelemewa na makonde mazito ya Changalawe huku akiwa ameshahesabiwa mara nane.
Kwa ushindi huo Changalawe ametinga hatua ya nusu fainali na kuihakikishia Tanzania na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupata medali.
Mashindano hayo ya Majeshi yalifunguliwa rasmi Novemba 20, katika Uwanja wa Taifa wa Moshood Abiola katika mji mkuu wa Abuja, Nigeria na yatafikia tamati Novemba 30, 2024.