Ligi Kuu

Kocha Baraza: Tunamini kesho tutavuna alama 3 za kwanza

DAR ES SALAAM: KOCHA wa Pamba ya Mwanza, Fransis Baraza, amesema timu yake ipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania, huku akisisitiza kuwa wamejipanga kikamilifu kupambana ili kupata ushindi wa kwanza na kujivunia alama 3.

Baraza amesema mchezo huo ni muhimu kwa timu yake kutokana na kutokuwa na kuwa na alama 1 tu! Katika michezo minne iliyopita, hivyo wameweka mkazo mkubwa kuhakikisha wanapata ushindi wao wa kwanza.

“Wachezaji wangu wanajua sisi ni timu ambayo bado hatujapata alama tatu katika mechi zote nne tulizocheza. Vijana wangu wanatambua hilo na ninaamini hatuna uoga. Tulichokifanya kwenye uwanja wa mazoezi ndicho tutakachokifanya uwanjani,” amesema Baraza.

Kocha huyo pia amesema hana sababu ya kuwalaumu wachezaji wake kwa matokeo yaliyopita, akieleza kuwa wamekuwa wakitekeleza maelekezo anayowapa wakati wa maandalizi ya michezo.

“Siwalaumu chochote wachezaji wangu kwa sababu wamefanya yote niliyowaagiza. Alama ni sehemu ya mchezo, ninaamini wataendelea kutekeleza ninayowaelekeza na katika mchezo wa kesho tunaamini tutapata alama tatu,” amesema.

Pamba sasa inaingia katika mchezo huo ikiwa na dhamira ya kubadili mwenendo wa matokeo na kuondoka uwanjani na alama tatu muhimu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button