Ligi Kuu

Kocha JKT Tanzania: Tutacheza na Pamba bila kujali alama walizonazo

DAR ES SALAAM:KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmed Ali, amesema timu yake itaingia uwanjani kucheza dhidi ya Pamba FC bila kujali idadi ndogo ya alama ilizonazo, akisisitiza kuwa wapinzani wao wana uwezo wa kushangaza katika mchezo huo.
Ahmed amesema katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Meja Isamuyo, Jijini Dar es Salaam utaikutanisha JKT Tanzania ikiwa na mawazo chanya ya kupata ushindi na kuongeza alama muhimu zitakazowasaidia kujiweka katika nafasi nzuri kiushindani.

Ahmed amesema licha ya Pamba kuwa na alama moja, JKT Tanzania haitafanya makosa ya kuwadharau, kutokana na ubora wa benchi lao la ufundi na uwezo wa wachezaji wao.

“Pamba wana mwalimu mzuri mwenye mbinu nyingi za kimchezo, hivyo wana uwezo wa kushinda. Tunachotakiwa sisi ni kuwa makini na kutimiza malengo yetu tuliyojiwekea na tulivyojipanga kuelekea mechi hiyo,” amesema Ahmed Ali.

Kocha huyo amesema maandalizi ya timu yake yamejikita katika kuhakikisha wanapata matokeo mazuri, huku wachezaji wakitakiwa kuzingatia maelekezo ya benchi la ufundi kwa muda wote wa mchezo.

JKT Tanzania sasa inaelekea kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kuongeza alama ili kujiimarisha zaidi katika msimamo wa ligi, huku Pamba nayo ikisaka ushindi wa kwanza wa alama tatu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button