Kamungo arejeshwa Taifa Stars

DAR ES SALAAM:MSHAMBULIAJI Bernard Kamungo amerejeshwa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki michezo ya kufuzu Kombe la Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar, pamoja na mchezo wa kirafiki dhidi ya Ghana.
Kamungo, anayekipiga katika klabu ya FC Dallas ya Marekani, aliwahi kuitwa katika kikosi cha Taifa Stars huko nyuma, lakini hakupata nafasi ya kucheza.
Baadaye alionekana akiiwakilisha timu ya vijana ya Marekani, jambo lililozua maswali kuhusu uwezekano wa kurejea kuichezea Tanzania.
Hata hivyo, jina lake limeonekana katika kikosi cha awali cha wachezaji 40 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi.
Mbali na Kamungo, wengine waliojumuishwa ni Aishi Manula, Zuberi Foba, Yona Amosi, Metacha Mnata na Hussein Masalanga.
Novatus Miroshi, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum, Lameck Lawi, Sheikhan Khamis, Morice Abraham, Twalib Nuru, Abdulkarim Kiswanya, Vedastus Masinde na Mohammed Mussa.
Wengine ni Pamoja na Danillo Maino, Haji Mnoga, Tarryin Allarakhia, Bakari Msimu, Nickson Kibabage, Mohammed Hussein, Anthony Mligo, Pascal Msindo, Abdul Suleiman, Nathaniel Chilambo, Cyprian Kachwele na Said Khamis.
Pia, kuna Himid Mao, Yona Amos, Adolph Mtasingwa, Yusuf Kagoma, Mohamed Sagaf, Alphonce Mabula, Charles Mmombwa, Seleman Mwalimu, Kelvin John na Paul Peter.




