Ligi KuuNyumbani

KMC kusuka au kunyoa leo

TIMU ya KMC leo itashuka katika dimba la Uhuru Dar es Salaam kuivaa Mbeya City katika mchezo wa mkondo wa pili wa mtoani wa kutafuta kusalia ligi kuu kwa msimu ujao.

KMC inaingia kwenye mchezo huo ikiwa nyuma baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa mabao 2-1 uliopigwa dimba la Sokoine.

Afisa habari wa KMC Christina Mwagala amesema wapo katika kipindi kigumu mno hivyo ni lazima waungane ili kuibakisha timu ligi kuu.

“Mchezo wa leo ni zaidi ya vita, tulishapanga mipango ya msimu ujao sasa ni lazima tubaki ligi kuu ili tuitekeleze” amesema Mwagala.

Mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atasalia ligi kuu huku timu itakayoshindwa ikicheza mchezo mwingine wa mtoano dhidi ya Mashujaa ya Kigoma ili kujua ni nani anakwenda Ligi kuu kwa msimu ujao.

Related Articles

Back to top button