Europa
Kinda Hispania aweka rekodi

KIJANA Lamine Yamal kutoka klabu ya Barcelona amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao akiwa na timu ya taifa ya Hispania katika ushindi wa mabao 7-1 kufuzu mashindano ya Euro 2024 dhidi ya Georgia jana.
–
Yamal, mwenye umri wa miaka 16 na siku 57 alifunga dakika ya 74 baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Dani Olmo kabla ya mapumziko.
–
Alvaro Morata alifunga hat-trick huku Solomon Kvirkvelia akijifunga na mabao ya Olmo na Nico Williams yakikamilisha ushindi huo.
–
Yamal ameweka rekodi ya mchezaji mdogo zaidi iliyowekwa na Gavi, ambaye alikuwa na umri wa miaka 17 na siku 62 alipocheza kwa mara ya kwanza Hispania mnamo 2021.