Europa

Umafia wa timu za Hispania Fainali

Timu kutoka taifa la Hispania zimeendelea kuonesha ubabe kwenye fainali za michuano mbalimbali Ulaya.

Timu ya Sevilla imehakikisha historia ya timu kutoka Hispania ya kutopoteza kwenye mchezo wa fainali inakuwa salama baada ya kuisambaratisha As Roma kwenye fainali ya Europa jana usiku.

Timu kutoka Hispania hazijapoteza mchezo wa fainali ya michuano ya Ulaya zinapokutana na timu kutoka mataifa mengine tangu mwaka 2001.

Hii ni mara ya Saba Sevilla wanatwaa ubingwa wa Europa ndani ya misimu 18 ya michuano hiyo.

Ubingwa wa Sevilla Umemfanya kocha wa Roma Jose Mourinho kupoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa fainali kwenye michuano ya Ulaya

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button