Kikosi Taifa Stars FIFA Series hiki hapa

Kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kitakachokwenda Azerbaijan kwa ajili ya michezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) Series 2024 kimetangazwa.
Wachezaji wa kikosi hicho kitakachokuwa chini ya kocha Hemed Morocco ni kama ifuatavyo:
MAGOLIKIPA: Aishi Manula, Aboutwaleeb Mshery na Kwesi Kawawa.
MABEKI: Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad, Lusajo Mwaikenda, Haji Mnoga, Mohamed Hussein, Novatus Dismas, Kennedy Juma na Miano Danilo.
VIUNGO: Feisal Salum, Mudathir Yahya, Morice Michael, Himid Mao, Yahya Zaydi na Tarryn Allarakhia.
WASHAMBULIAJI:
Clement Mzize, Saimon Msuva, Kibu Denis, Abdul Suleiman, Ben Starkie na Charles M’mombwa.
Katika michuano hiyo iliyopangwa kufanyika Machi 22 hadi 25 katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku Taifa Stars itacheza na Bulgeria na Mongolia.