Ligi Kuu
Kayoko apewa tena Dabi
MWAMUZI, Ramadhan Kayoko amepewa jukumu la kusimamia sheria za mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Vs Yanga utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.
Taarifa kutoka bodi ya ligi imeeleza kuwa Kayoko atasaidiwa na Mohamed Mkono na Kassim Mpanga, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo.
Imepita muda mrefu tangu mwamuzi huyo asimamie mchezo huo mkubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, ambapo kwa siku za hivi karibuni waamuzi Elly Sasii na Ahmed Aragija walitawala kusimamia katika mchezo huo.