Ligi KuuNyumbani

Ushindani umeongezeka Ligi Kuu-Maxime

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kwa muda wa misimu miwili na nusu aliyokaa pembeni ushindani kwenye Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara umeongezeka zaidi hivyo ni lazima atumie mbinu bora na za kisasa katika klabu yake ili kumudu mapambano.

Maxime alirejea kuwa kocha Kagera Sugar Oktoba 30,2022.

Akizungumza na SpotiLeo ameahidi kufanya vizuri kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu kwani anakusudia kufanya maboresho kwenye dirisha dogo.

“Nimepanga kuongeza wachezaji kama wiwili mshambuliaji mmoja na beki wa kati mmoja na baada ya hapo nitaanza kupandikiza mifumo yangu ambayo ndiyo nataka wachezaji waitumie,” amesema Maxime.

Amesema pamoja na wachezaji wa Kgaera Sugar kucheza kwa kujituma na kuipigania timu hiyo kuna mapungufu amepanga kuanza kuyafanyia kazi.

Kagera Sugar inashika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 13.

Related Articles

Back to top button