Habari Mpya

Kanu yupo Bongo bwana!

DAR ES SALAAM:Mchezaji Kutoka Nchini Nigeria ambaye pia ni Mkongwe kwenye kulisakata kabumbu aliyejizolea umaarufu kupitia timu ya Arsenal Nwankwo Kanu ametua nchini Tanzania kusaidia watoto wenye matatizo ya Moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Tanzania Foundation, Zeweina Farah amesema kuwa mchezaji huyo wa zamani amekuja kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye changamoto ya Moyo.

“Kesho anatarajia kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Mloganzila kwa kuwatembelea na kuwasalimia ili kuwasaidia watoto wenye matatizo moyo kuangalia jinsi ya kuwasaidia kupata matibabu.”

” Atakuwepo na shughuli yake itakayofanika siku ya jumapili katika viwanja vya Coco beach ili kukutania na wachezaji na watu mbalimbali watakaosaidia na kucheza michezo mbalimbali.”amesema Zuweina

Kwa upande wake Mchezaji huyo amesema yupo tayari kushirikiana na watanzania na kuwasaidia watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wanahitaji matibabu.

Related Articles

Back to top button