Joao Palhinha katika radi za Bayern
TETESI za usajili zinaeleza kuwa Bayern Munich itakabiliana na ushindani kutoka kwa angalau vilabu viwili vya Ligi Kuu England Januari 2024 katika kumsajili kiungo wa Fulham mreno Joao Palhinha, 28.(Telegraph – subscription)
Newcastle United inaweza kusajili wachezaji watano Januari 2024 huku nafasi ya golikipa ikiwa kipaumbele.(Sun)
Aston Villa inasema ili timu inayotaka kumsajili kiungo wake mbrazil Douglas Luiz Januari 2024 italazimika kutuma ombi la pauni milioni 60, huku Arsenal ikiendelea kuonesha nia.(Caught Offside)
Villa imeweka thamani ya Luiz kuwa pauni milioni 110.(Football Transfers)
Real Sociedad ya Hispania inapigiwa chapuo kumsajili fowadi wa Manchester United na England, Mason Greenwood, 22, ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Getafe.(Todofichajes – in Spanish)
Kiungo mdachi anayekipiga Manchester United, Donny van de Beek ameomba kusajiliwa Barcelona kama mbadala wa majeruhi Gavi.(Sport – in Spanish)