Tetesi

Ishu ni Aziz? Tulieni

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imeahidi ‘kuvunja benki’, kwa kutoa dau analolihitaji nyota wao Stephane Azizi Ki aendelee kusalia ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano.

Mkataba wa Yanga na Aziz Ki umefikia tamati na klabu kwenye mazungumzo pande zote mbili kwa ajili ya kuhakikisha wanafanikiwa kumuongeza mkataba mwingine kutumikia klabu hiyo.

Imeelezwa kuna klabu mbalimbali ikiwemo kutoka Afrika Kusini, Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns na Pyramids kutoka kaskazini mwa Afrika kutuma ofa ya pili ya dola laki 500 kwenye menejimenti ya kiungo huyo.

Pyraminds imetuma ofa hiyo rasmi kwa watu wanaomsimamia mchezaji huyo ili kupata saini ya kiungo mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na msimu bora sana.

Aziz Ki bado hajasaini mkataba mpya mpaka sasa lakini ameipa kipaumbele kikubwa klabu hiyo kusaini mkataba mpya, muafaka rasmi wa Aziz Ki na Yanga utafikiwa hivi karibuni upo katika hatua za mwisho baada ya majukumu ya timu ya Taifa.

Akizungumza na Spotileo, rais wa Yanga injinia Hersi Said amesema hawako tayari kuona kiungo huyo anaondoka ndani ya timu hiyo kwa kuhakikisha wanambakiza kwa kumuongezea mkataba kwa kumpa dau ambalo amelihitaji katika mazungumzo ya kwanza.

Amesema kulingana na mipango yao kuona Yanga inafikia malengo ya kucheza fainali ya Afrika wanahitaji kuendelea kuwabakiza nyota wenye ubora akiwemo Aziz Ki na wengine na baadaye wanaanza kuangalia nyota wapya.

“Niwaahidi mashabiki na wanachama tutafanya usajili mkubwa sana msimu ujao tutafanya mambo makubwa kuanzia ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, tutafanya ‘pre seasons’ nzuri, tumepata mialiko maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini (Kaizer Chief). Mh, Raila Odinga ametuomba tuungane kwenye uzinduzi wao huko Kisumu pamoja na nchini moja ya Ulaya,” amesema Hersi.

Amesema klabu inahitaji kujengeka kiuchumi kazi yao kama viongozi ni kuhakikisha wanapata wadhamini ambao watasaidiana na mfadhili wao GSM, lakini mashabiki wao pia wanao mchango mkubwa kwa kuhakikisha kuwa Kupitia ada za Wanachama wanapata mapato ya kuendeleza klabu hiyo.

“Tumefanikiwa kurejea hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya miaka 25, watu wengi walidhani kuwa hatutaweza kufika hatua ya robo fainali kwa sababu tulikuwa kwenye kundi gumu sana, lakini tukawashangaza wale waliotukatia tamaa.

Tulifanikiwa kutinga hatua ya robo fainaliu na kutolewa kwa matuta na Bingwa wa AFL na kigogo wa soka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns, hata hivyo katika mchezo tulifunga bao halali, rais wa soka Afrika, Dr Patrice Motsepe amenukuliwa akisema kuwa lilikuwa goli la halali,” amesema Hersi.

Related Articles

Back to top button