Mastaa

Angelina Jolie kupiga mnada Ferrari yake

NEW YORK: MUIGIZAJI Angelina Jolie ameweka sokoni gari lale la Ferrari 250 GT ambalo ni toleo la 1958.

Gari hilo limepangwa kupigwa mnada mjini Paris na bei iliyowekwa katika kuliuza ni kati ya pauni 600,000 na 800,000 na litauzwa katika uuzaji wa kipekee wa Christie, Novemba 20.

Ingawa gari hilo huhifadhi injini yake ya asili, inaelekea lilipakwa rangi upya mwaka wa 1978 kutoka rangi yake ya awali nyeupe na bluu hadi nyeusi, huku mambo ya ndani yakibadilika kutoka nyeusi hadi nyekundu.

Kwa mujibu wa mtandao wa odometer gari hilo limetembea maili 64,244, mitambo ya gari na asili yake bado haijawekwa wazi.

Kwa mujibu wa Christie uuzaji wa gari hilo unatarajiwa kupanda zaidi ya bei ya awali ambayo ni kati ya pauni 600,000 hadi 800,000.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button