EPL

Ishu ya Marmoush kutua Man City imenyooka

MANCHESTER:MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester city wako karibu kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Omar Marmoush ikielezwa kuwa tayari wababe hao wa jiji la Manchester wamekubaliana masuala binafsi na mchezaji huyo na sasa suala liko upande wa klabu yake ya Frankfurt.
Taarifa za kuaminika kutoka jijini Frankfurt zinasema kuwa mchakato rasmi wa kumhamishia EPL Marmoush huenda usiwe mgumu kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Eintracht Frankfurt na Manchester City.
Marmoush mwenye miaka 25 ni wa pili kwenye orodha ya wapachika mabao wa Bundesliga akiwa na mabao 13 katika michezo 15 nyuma ya Harry Kane mwenye mabao 14 akiwa pia na asisti 7 huku akiisaidia klabu yake kushinda mechi 8 na kukaa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Bundesliga wakiwa na pointi 27
Manchester City wapo katika harakati za kukiboresha kikosi chao na sasa jicho lao limeelekea kwa Marmoush mwenye uraia pacha wa Egypt na canada ambaye amekuwa na kiwango bora msimu huu huku pia wakikomaa na beki wa Lens ya Ufaransa Abdulkodir Khusanov na Mbrazil Vitor Reis kutoka Palmeiras katika dirisha kubwa la usajili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button