Habari Mpya

Ishu ya Kagoma: Magori nae ndani

DAR ES SALAAM: Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba Sports club Crescentius Magori ameliomba shirikisho la soka nchini TFF kuchukua hatua dhidi ya kile alichodai upotoshaji wa wazi uliofanywa mapema leo hii na watani wao wa jadi Yanga sc

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Magori ameikumbusha TFF kutoa adhabu kwa klabu hiyo kama ilivyofanya kwa kiongozi wa zamani wa klabu hiyo Marehemu Hans Pope ambaye aliwahi kuadhibiwa kwa kuzungumza sakata la Benard Morrison ambalo kwa wakati huo lilikuwa kwenye Kamati ya Sheria.

Magori amesisitiza kuwa Simba haijawahi kupata barua yoyote ya Kagoma kusimamishwa kucheza kama alivyoeleza mwanasheria wa klabu ya Yanga Patrick Simon.

Mapema leo hii klabu ya Yanga kupitia kwa mwanasheria wao Patrick Simon waliwaeleza waandishi wa habari mambo mbalimbali yanayohusu sakata la usajili wa mchezaji huyo na kudai kuwa ni mali ya klabu hiyo

Simon aliyeambatana na msemaji wa klabu hiyo Ally Kamwe walionesha vielezo mbalimbali kuthibitisha madai ya mchezo Yusuph Kagoma kusaini na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC.

Related Articles

Back to top button