Sadio Kanouté apewa mkono wa kwaheri Simba SC
ISMAILIA: UONGOZI wa klabu ya Simba umeamua kuachana na kiungo wao mkabaji, Saidio Kanoute baada ya mkataba wake kufikia tamati na kutokuwa kwenye mipango ya timu hiyo kwa msimu wa 2024/25.
Taatifa ya kuachwa kwa kiungo huyo mvunja kuni imetolewa leo Julai 9 saa 10 jioni, hapo awali Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa kuelekea maboresho ya msimu mpya wa 2024/25 wa mashindano, klabu hiyo itaachana na baadhi ya nyota na Kanoute ni mmoja wao.
Sadio Kanoute alijiunga na Simba msimu wa 2021/22 kutoka klabu ya Al Ahly Benghazi ya libya kwa miaka mitatu, kiungo huyo ambaye amekuwa na uhusiano mzuri na viongozi na wachezaji amekuwa akijotoa katika muda wote wa mchezo na kuhakikisha anasaidia timu hiyo kupata ushindi.