Ibenge alia na Uwanja wa Sokoine

MBEYA: KOCHA Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema ni vigumu kucheza mpira mzuri kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kutokana na hali ya uwanja huo, baada ya timu yake kutoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons jana.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Ibenge amesema aina ya uwanja huo inafanya timu ishindwe kucheza mpira wa pasi na kulazimika kupiga mipira mirefu mara nyingi.
“Ni vigumu kucheza kwenye aina hii ya uwanja, hivyo tumekuja hapa na kuondoka bila kufungana. Unapocheza katika mazingira kama haya huwa hauchezi mpira wa miguu wa kawaida, unalazimika kupiga mateke zaidi,” amesema.
Hata hivyo, Ibenge amesema hawalalamiki kuhusu matokeo hayo akisisitiza kuwa wamepata pointi moja muhimu katika mbio za ubingwa.
“Hatukufanya hivyo na hatulalamiki. Huu ni ubingwa na tumepata pointi moja, tunashukuru,” amesema kocha huyo.




