Kwingineko

Gerrad yamemshinda Saudia

RIYADH: KOCHA wa Al Ettifaq na Mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England Steven Gerrard ameondoka klabuni hapo kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kudumu klabuni hapo kwa miezi 18.

Meneja huyo wa zamani wa Aston Villa alisaini ongezeko kwenye mkataba wake kwa miaka miwili zaidi mkataba ambao ungemuweka nchini Saudi Arabia mpaka 2027 lakini hali mbaya ya matokeo ya klabu hiyo hivi karibuni ikishinda mechi 5 pekee kati ya 17 zilizowaacha pointi 5 juu ya mstari wa kushuka daraja imemuondoa.

“Wakati mwingine mpira ni mchezo usiotabirika na mambo huwa hayaendi tunavyotaka. Hata hivyo ninaondoka kwa heshima kwenye klabu hii na nchi hii nzuri, sina shaka kazi nzuri inayoendelea hapa itazaa matunda na nawatakia heri” amesema Gerrard

Rais wa Al Ettifaq Same Al Misehal amemshukuru Gerrard na kusema kuwa amesaidia kuibadilisha klabu hiyo katika kipindi chake cha mwaka mmoja na nusu klabuni hapo na amesaidia kujenga msingi wa mafanikio kwenye klabu hiyo baadaye.

“Ameibadilisha sana klabu hilo halitasahaulika, maamuzi haya yamefikiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili kwa maslahi mapana ya wote” amesema

Gerrard alijiunga na klabu hiyo ya ligi kuu ya Saudi Arabia, Saudi Pro League Julai mwaka 2023, akiikuta klabu hiyo kwenye nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na anaondoka klabu hiyo ikiwa nafasi ya 12 akishinda michezo mitano pekee msimu huu.

Related Articles

Back to top button