Nyumbani

Gamondi: tupo tayari kucheza na Liechtenstein

KIGALI, Rwanda: KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo tayari kuanza vyema michuano ya FIFA Series kwa kucheza soka kuvutia na lenye matokeo watakaposhuka dimbani dhidi ya Liechtenstein leo nchini Rwanda.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo huo wa kimataifa saa 11:30 jioni, huku pambano la ufunguzi wa michuano hiyo likitarajiwa kuchezwa saa 8:30 mchana.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Gamondi amesema benchi la ufundi limeendelea kufanya kazi ya kuboresha maeneo ya kiufundi na kimkakati ili kuhakikisha timu inaingia uwanjani ikiwa na mfumo sahihi kulingana na aina ya mpinzani watakayekutana naye.

Amesema katika maandalizi hayo, kipaumbele kimekuwa ni kuijenga Taifa Stars katika mfumo wa uchezaji utakaosaidia timu kucheza kwa ubora huku ikiongeza nafasi ya kupata ushindi.

“Tunafanya kazi ya kuboresha masuala ya kiufundi na namna ya kucheza kulingana na mpinzani tuliyenaye. Lengo ni kuwa na timu inayocheza vizuri na yenye ushindani,” amesema Gamondi.

Kocha huyo pia amegusia matarajio makubwa ya mashabiki wa Tanzania, akieleza kuwa anaelewa vizuri hamasa waliyonayo kwa Taifa Stars kila inapokuwa kwenye majukumu ya kimataifa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa katika soka hakuna anayeweza kuahidi matokeo moja kwa moja, lakini jambo ambalo timu yake inaweza kuliahidi ni kupambana kwa nguvu zote, kuonesha nidhamu, umakini, kujitoa na ari ya ushindi ndani ya uwanja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button