Nyumbani

Chamazi ‘kuhost’ Sudan Super League

DAR ES SALAAM: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu nchini Sudan (SFA) wakiomba Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano yao ya Sudan Super League yanayoshirikisha jumla ya timu 3.

Sudan Football Association (SFA) wameomba kucheza michezo hii hapa nchini katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ikiwa ni sehemu ya kurudisha Amani nchini kwao kufuatia kuwepo kwa machafuko ya kisiasa yaliyopelekea kushindwa kuandaa michezo/mashindano ya ligi nchini kwao.

SFA wanaamini kupitia shindano hili itawasaidia wananchi wa Sudan kurudisha umoja wao na kufurahia kuona timu zao zikicheza tena baada ya kutofanya hivyo kwa muda sasa.

Michezo ya Super League inatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 25 -30, 2024 ambapo kila siku kutakua na mchezo mmoja tu na muda wa michezo (kickoff) saa 12:00 jioni.

Timu zinazoshiriki shindano hilo ni Al Hilal SC, Al Merrikh na Al Wadi Nyala zote za Sudan.

Ratiba ya michezo hiyo ni kama ifuatavyo:

25.06.2024: Al-Hilal SC v Al-Wadi Nyala (saa 12:00 jioni)

27.06.2024: Al-Wadi Nyala v Al Merrikh SC (saa 12:00 jioni)

30.06.2024: Al-Marikh SC v Al-Hilal SC (saa 12:00 jioni)

Related Articles

Back to top button