BurudaniFilamu

Filamu ya Eonii Gumzo kila kona

FILAMU ya Eonii iliyoongozwa na Mtanzania Eddie Mzale imeendelea kuzungumzwa kwenye maeneo mbalimbali  na kumwagiwa sifa lukuki.

Filamu hiyo ambayo imeshinda tuzo ya filamu bora ya Tamasha la 26 la ZIFF lilofanyika Zanzibar imeibua wadau mbalimbali wa Filamu hapa nchini.

Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF Prof. Martin Mhando amesema ujio wa filamu hiyo una maana kubwa kwenye tasnia ya filamu nchini na hivyo inaamsha zaidi wasanii kufanya kazi kwa ubora.

“Hii ni alama kubwa ya kukua kwa tasnia ya filamu nchini , filamu hii imetuheshimisha kama filamu ya Binti ya Vuta N’kuvute ilivyofanya vizuri amesema Prof Mhando.

Ushindi wa Filamu hiyo katika Tamasha la ZIFF unakuwa ni ushindi wa tatu mfululizo kwa filamu za Tanzania kushinda tuzo ya filamu bora kwenye tatamsaha hilo ambapo jumla ya filamu 2,810 kutoka mataifa 32 duniani zilikuwa katika kinyanga’anyiro hicho.

Related Articles

Back to top button