Ligi Kuu

Fadlu ndio kila kitu Simba

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kocha Fadlu Davids amehusika kwa asilimia 100 kwenye usajili wa wachezaji wa timu hiyo akiwemo mshambuliaji mpya Ellie Mpanzu.

Jumatatu Septemba 30, saa 5 usiku Simba imemtambulisha aliyekuwa mchezaji wa klabu ya As Vita ya DR Congo, Mpanzu kwa mkataba wa miaka miwili na leo ameingia kambini na timu hiyo kujiandaa na michezo iliyopo mbele yao.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wamethibitishiwa na Kocha Fadlu kuwa ameshiriki katika kila hatua ya usajili uliofanywa wa Simba.

“Tuliingia makubalino na Kocha Fadlu mapema tulishindwa kumtambulisha mapema kwa sababu alikuwa na mkataba na timu ya awali lakini kipindi chote alikuwa akishiriki katika usajili hata Mpanzu alikuwa chaguo lake la kwanza,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa Mpanzu alikuwa kwenye mipango yao ya muda mrefu, kutokana na changamoto zilizokuwepo nje ya uwezo wao na wamefanikiwa kupata huduma ya nyota huyo.

 

Related Articles

Back to top button