Tetesi

Enzo Fernandez kuondoka Chelsea iwapo…

KIUNGO wa kati Enzo Fernandez atafikiria kuondoka Chelsea The Blues’ hivi karibuni iwapo klabu hiyo itaendelea kusuasua, akiwa amekatishwa tamaa na ubora wa The Blues tangu aliposajiliwa kutoka Benfica Januari mwaka huu.(Fichajes)

Baada ya kushindwa kumsajili kiungo wa Fulham, Joao Palhinha katika kipindi cha majira ya kiangazi, Bayern Munich tayari inapanga kurejea kumsaka kiungo huyo mwezi Januari, 2014. (Fabrizio Romano)

Mohamed Salah hataondoka Liverpool mwaka huu na atakataa nafasi ya kupata kandarasi yenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 400 sawa na shilingi trilioni 1.25.

Eric Dier amefanya mazungumzo ya dharura na mwenyekiti wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy baada ya kutochezeshwa kikosi cha kwanza chini ya kocha mpya Ange Postecoglou.(Telegraph)

Barcelona inapanga kusajili kiungo wa kati wakati wa dirisha dogo la uhamisho Januari 2014, huku Jorginho wa Arsenal akiwa miongoni mwa majina yanayofikiriwa.(Mundo Deportivo)

Related Articles

Back to top button