Tetesi
Gabri Veiga apambanisha vigogo England

MABINGWA wa Ligi Kuu England, Manchester City imeingia katika mbio za kusaka saini ya kiungo wa Celta Vigo ya Hispania Gabri Veiga baada ya kujitoa kwenye dili la Declan Rice.
Veiga pia anawaniwa na Liverpool na Chelsea na ana kipengele cha kuachiwa cha pauni milioni 34.6 sawa na shilingi bilioni 102.2.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye hucheza hasa namba 6 au 8 yupo katika orodha ya City ya wachezaji wanaohitajika wakati mabingwa hao wa EPL, FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya wakijiimarisha baada ya kumpoteza İlkay Gündoğan aliyehamia Barcelona na kumkosa Rice.
Veiga amefunga magoli 11 na kutoa pasi 4 za magoli katika michezo 36 ya La Liga msimu uliopita.