Tetesi

Waziri Junior anyoosha melezo ‘ishu’ ya Ihefu

JAKARTA. MSHAMBULIAJI wa KMC FC, Waziri Junior amefunguka kuhusishwa na kujiunga na Ihefu FC kuwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spotileo, Waziri JR amekiri kuwepo na mazungumzo na Ihefu FC lakini pamoja na timu yake ya Ihefu FC, kuhakikisha wanambakiza ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao.

Amesema kwa sasa anaipa kipaombele timu yake ya KMC FC, wameonyesha nia ya kumbakiza kikosini lakini pia mazungumzo ya Ihefu FC yanaendelea na kufikia asilimia 50.

“Kwa sasa ni mapema kusema msimu ujao nitakuwa wapi, hadi sasa nina ofa mbili ambayo ni KMC FC timu yangu lakini na Ihefu FC, tunaendelea na mazungumza na yapo 50 kwa 50,” amesema mshambuliaji huyo.

Waziri Junior ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kilichorejea leo nchini akitokea Indonesia ambapo walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao ikiwa ni maandalizi ya mchezo ya kufuzu ushiriki wa kombe la Dunia, dhidi ya Zambia.

Mshambuliaji huyo amepita kwenye timu mbalimbali ikiwemo Dodoma Jiji FC,Azam FC pamoja na Yanga kwa misimu tofauti tofauto na msimu huu amemaliza ametumikia KMC FC.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button