Dube: Msimu ujao uhakika Ligi Kuu
MOROGORO: Aliyekuwa Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube ameweka wazi kuwa atakuwa ni miongoni mwa wachezaji watakaocheza katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2024/25.
Dube aliyeingia sintofahamu na uongozi wa Azam FC kwa kuvunja mkataba wake katikati ya msimu wa 2023/24, anahusishwa na klabu mbili kubwa nchini,Simba na Yanga.
Mshambuliaji huyo ni sehemu ya kikosi cha timu Dickson Job katika tamasha la WAPE TABASAMU litakalofanyika katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Akizungumza na Spotileo, Dube amesema amerejea nchini kuja kuwaunga mkono wachezaji wenzake katika tamasha la wape tabasamu liloandaliwa na nyota wa Yanga, Kibwana Shomari na Dickson Job.
Amesema ni muda mrefu hajacheza mpira hivyo mechi hiyo itamsaidia kujiweka vizuri na kufurahia na wachezaji wenzake Pamoja na kufikisha ujumbe kwa jamii.
“ Nimefurahi kurejea na kuungana na wachezaji wenzangu katika kufanikisha jambo lao. Nitarudi na kucheza soka Tanzania, timu gani?, basi itajulikana baadae,” amesema Dube.